Utabiri Kombe la Dunia

Translated into Swahili (Original version)


Je, unamkumbuka pweza Paul? Alikuwa nyota wa Kombe la Dunia 2010, kwa kuwa na uwezo wa kutabiri mshindi wa mechi za Ujerumani. Pia alitabiri mshindi wa mchezo wa mwisho. Kazi yake ilianza na Euro 2008, na aliendelea kutabiri kiusahihi mechi 11 kati ya 13. Alikuwa akichagua kati ya masanduku mawili yenye chakula na bendera ya taifa ya kila timu iliyoshiriki katika kila mechi. Kwa bahati mbaya, alikufa mwishoni mwa 2010.

Paul hakuwa peke yake. Hata mamba Harry alitabiri mshindi wa Kombe la Dunia 2010. Zaidi ya hayo, aliweza kutabiri mara mbili mfululizo matokeo ya uchaguzi ya Shirikisho la Australia . Hata hivyo, yeye kamwe hakuwa na mvuto kama wa pweza wa Ujerumani. Wala Mani hakufanya vizuri zaidi, kasuku wa Singapore ambaye alitabiri robo na nusu fainali zote za Kombe la Dunia 2010, kwa sababu alishindwa kubashiri nani angefanikiwa kati ya Hispania na Uholanzi katika fainali.

Tangu kuondoka bila kutegemewa kwa Paulo, kumekuwa na ushindani mkubwa juu ya nani wa kuchukua taji lake. Wakati wa Euro 2012, kulikuwa na wanyama watatu waliokuwa wakicheza mchezo huu: Citta, tembo toka India anayeishi katika eneo la kufuga wanyama mjini Krakow, Poland. Fred, paka fereti wa Kiukreni ambaye anaweza kufuatiliwa kwenye Twitter. Na Funtik, nguruwe wa Kiukreni anayetumika kupiga ramli mwenye uwezo wa kutabiri kiusahihi mechi 2 kati ya 3.

Nani atachukua nafasi ya pweza Paul wakati wa Kombe la Dunia lijalo? Je, ni kasuku aliyebarikiwa na Papa Francis katika eneo la Mtakatifu Petro, ambaye sasa ni nyota wa stesheni ya kitaifa ya utangazaji kwa umma nchini Italia? Au atakuwa Nelly, tembo wa Ujerumani ambaye ametabiri kwa usahihi mechi 30 kati ya 33 hadi sasa? Na bila shaka, usidharau uwezo wa panda mtoto anayeungwa mkono na vyombo vya habari vya kiserikali vya Kichina.

Kasuku wa Kitaliano aitwaye Amore (Upendo kwa Kitaliano) atatoa utabiri wake kwa kuchagua bendera ya timu itakayoshinda kwenye uwanja mdogo wa mpira wa miguu. Nelly anapendelea kutabiri washindi kwa kupiga mateke mpira kuingia ndani ya mmojawapo ya nyavu yenye bendera ya nchi zinazoshindana zilizowekwa mbele yao. Badala yake, panda mtoto atatabiri matokeo ya mechi kwa kuokota chakula kutoka katika masanduku yenye alama ya bendera wakati wa mechi za makundi na kwa kupanda mti wenye bendera katika raundi za mtoano.

Je, una ndege au mnyama unayemfuga?
Je, yeye anaweza kuwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi? Kivipi?
Waache wajaribu!

by Julius Kabyemera

3 Votes
#589 of #1440 in the World
#2 of #3 for SwahiliGo to the ranking page for Swahili

Can you translate better?

Join the challenge